LONDON: Watuhumiwa 10 wazuiliwa nchini Uingereza
11 Agosti 2005Matangazo
Serikali ya Uingereza imewazuilia raia kumi wa kigeni wanaotuhumiwa kuwa hatari kwa usalama wa taifa. Msemaji wa wizara ya mambo ya ndani nchini humo amekataa kuyataja majina ya washukiwa hao lakini akasema watarudishwa nchini kwao.
Juma lililopita waziri mkuu wa Uingereza bwana Tony Blair alitangaza sheria kali zinazolenga kuirihusu serikali yake kuwarudisha nchini kwao waislamu wenye itikadi kali. Hatua ya kuwazulia washukiwa hao imefanyika mwezi mmoja baada ya mashambulio ya mabomu ya Julai saba mjini London, yalioyosababisha vifo vya watu zaidi ya 50.