LONDON: Uingereza imevutiwa na treni ya Kijerumani „Transrapid“
7 Juni 2005Matangazo
Ripoti zasema kuwa serikali ya Uingereza inafikria kujenga njia ya reli itakayotumia treni ya Kijerumani „Transrapid“ kuiunganisha miji ya London na Glasgow.Inasemekana kuwa mawaziri wa serikali ya Uingereza wamevutiwa na huduma za treni hiyo ya Kijerumani katika uwanja wa ndege wa Shanghai nchini Uchina.Kampuni ya Transrapid imesema,gharama ya njia ya reli iliyopendekezwa kati ya London na Glasgow itakuwa kama Euro bilioni 23.7.Treni hiyo inafikiriwa pia kutumiwa katika uwanja wa ndege wa Munich nchini Ujerumani,uwanja wa ndege wa Pittsburg,Marekani na pia kati ya Baltimore na Washington na vile vile Las Vegas,California.