LONDON: uhusiano utaendelea kuwa mzuri baina ya Uingereza na Irak
22 Septemba 2005Waziri wa ulinzi wa Uingereza bwana John Reid na waziri mkuu wa Irak Ibrahim el Jafaari wamezimua makali ya ghasia zilizotokea kusini mwa mji wa Basra kufuatia hatua ya majeshi ya Uingereza ya kuwakomboa wenzao .
Waziri Reid na waziri mkuu el Jafaari wamewaambia waandishi habari mjini London kwamba hatua ya wanajeshi hao haitaathiri uhusiano baina ya nchi zao.
Mapema wiki hii askari wa Uingereza waliivamia jela moja katika mji wa Basra kwa lengo la kuwakomboa askari wenzao wawili waliotiwa ndani katika jela hiyo .
Askari hao walikamatwa na polisi ya Irak.
Lakini askari hao walikutwa katika nyumba ya mtu binafsi. Majeshi ya Uingereza yamedai kwamba askari hao walikuwa wanashikiliwa na wapinzani baada ya kupelekwa katika nyumba hiyo na mapolisi wa Irak.
Maafisa wa Irak wamekanusha madai hayo na kusema kwamba wanajeshi hao hawakutolewa jela na wala hawakupelekwa kwa wapinzani.
.