LONDON: Siku ya mwisho ya kampeini ya uchaguzi mkuu,Uingereza
4 Mei 2005Matangazo
Kampeini ya uchaguzi nchini Uingereza inamalizika leo huku uchaguzi mkuu ukitarajiwa kufanyika hapo kesho.
Katika kampeini hiyo Viongozi wa upinzani kutoka chama cha Conservative na Liberal Demokrats wamekuwa wakiwatolea wito wapiga kura kumuadhibu kutokana na kujiingiza katika vita vya Iraq. Chama cha Labour cha bwana Blair hata hivyo kinatarajia kushinda katika uchaguzi huo kutokana na kunadi sera zake kwa kuzungumzia mipango ya kiuchumi.
Kwa mujibu wa kura ya maoni,waziri mkuu Tony Blair anatarajiwa kuchaguliwa tena lakini kwa kura kidogo kutoka upande wa chama chake.