LONDON: Serikali ya Blair yatuhumiwa kuhusu vita vya Iraq
25 Machi 2005Matangazo
Serikali ya Uingereza upya imeshambuliwa kuhusika na uvamizi wa Iraq.Chama cha upinzani cha Kikonservativ kimeituhumu serikali kuwa ilimshinikiza Mwanasheria Mkuu kubadilisha maoni yake juu ya uhalali wa vita.Waziri wa mambo ya kigeni wa Uingereza Jack Straw anakataa kuichapisha hati ya mashauri yaliotolewa kwa serikali kabla ya kuanzishwa vita vya Iraq.Lakini tume huru ya uchunguzi inatazamiwa kuichunguza ripoti hiyo na kuamua ikiwa iwekwe siri kwa maslahi ya umma.