LONDON: Polisi wamuachilia mshukiwa wa njama ya kuzilipua ndege
17 Agosti 2006Matangazo
Polisi nchini Uingereza wamemuachilia huru mtuhumiwa mmoja aliyekamatwa wiki iliyopita kuhusiana na njama ya kutaka kuzilipua ndege za abiria kutoka Uingereza kwenda Marekani.
Hapo awali mahakama ya mjini London imewapa polisi muda zaidi kuendelea kuwahoji washukiwa 23 wa njama hiyo.
Hapo jana mawaziri wa mambo ya ndani wa Umoja wa Ulaya walionya katika mkutano wao mjini London kwamba Ulaya inakabiliwa na hatari kubwa ya mashambulio ya kigaidi.