LONDON: Polisi hawatoshtakiwa kuhusu Menezes
18 Julai 2006Matangazo
Maafisa wa polisi nchini Uingereza waliyompiga risasi na kumuua Mbrazil asie na hatia, hawatokabiliwa na mashtaka ya jinai.Polisi hao kwa makosa walidhania kwamba Jean Charles de Menezes alikuwa mshambulizi aliejitolea muhanga. Idara ya waendesha mashtaka-CPS iliyopewa jukumu la kuchunguza kesi hiyo imesema,idara ya polisi ya jiji la London,ndio itashtakiwa kwa kwenda kinyume cha sheria za afya na usalama.Mwaka jana, mjini London,Mbrazil huyo aliekuwa na umri wa miaka 27 alipigwa risasi kichwani mara saba na polisi,alipoingia ndani ya treni ya chini kwa chini.Msemaji wa ofisi maalum katika idara ya CPS amesema haukuwepo ushahidi wa kutosha kufungua mashtaka dhidi ya mtu maalum kuhusika na tukio hilo.