LONDON. Mtuhumiwa akata rufaa dhidi ya kurudishwa Uingereza
26 Agosti 2005Matangazo
Mtuhumiwa wa mashambulio ya mabomu viza ya julai 21 mjini London aliyekamatwa huko Roma Italia amekata rufaa dhidi ya amri inayomtaka arejeshwe nchini Uingereza.
Hamdi Issac mzaliwa wa Ethiopia ambae anajulikana pia kama Osman Hussein aliamriwa kurudihswa Uingereza na mahakama ya Italia mapema mwezi huu lakini mawakili wake wanasema kuwa hakuna ushahidi uliotolewa kuwa mteja wao alitenda uhalifu.
Issac mwenyewe amekiri kuwa alihusika katika mashambulio ya mtandao wa usafiri mjini London lakini akasisitiza kuwa mashambulio hayo hayakuwa na nia ya kuuwa bali kuzusha hofu tu miongoni mwa watu.
Alikimbilia nchini Italia baada ya kutokea shambulio jingine mjini London lililowauwa watu zaidi ya 50.