LONDON. majeshi ya Uingereza yamechoka nchini Afghanistan
6 Agosti 2006Matangazo
Majeshi ya Uingereza yanayoongoza mapigano dhidi ya wapiganaji wa kitaliban nchini Afghanistan yanasemekan kuwa yamechoka na yanahitaji kuongezewa nguvu.Gazeti la Daily Telegraph la Uingereza limeripoti hayo. Gazeti hilo limemkariri kamanda mmoja akisema kuwa askari wa Uingereza wameshakabiliwa na mapambano 25 tokea mwezi wa mei, katika jimbo la hatari kubwa sana la Helmand.
Jeshi la Uingereza nchini Afghanistan, lenye askari alfu 3 na mia tatu linahitaji kuongezewa nguvu kwa askari wengine alfu moja.