London. Majeshi ya Uingereza hayataondoka Iraq.
26 Septemba 2005Waziri mkuu wa Uingereza Tony Blair amekanusha ripoti kuwa majeshi ya nchi hiyo yataanza kuondoka kutoka Iraq May mwakani.
Akizungumza mwanzoni mwa mkutano wa siku tano wa chama cha Labour katika kitongoji cha Brighton mjini London, Blair amesema kuwa kuwepo kwa majeshi ya Uingereza nchini Iraq ni muhimu pia kwa maslahi ya usalama wa Uingereza.
Chama cha upinzani cha Liberal Democrats pamoja na wanachama wa mrengo wa shoto wa chama cha Labour wamedai kuwepo na mpango wa serikali wa kujiondoa kutoka Iraq. Wakati huo huo huko Iraq kiasi cha watu 17 wameuwawa katika matukio kadha ya milipuko ya mabomu ya kujitoa muhanga nje na ndani ya mji mkuu Baghdad.