London. Maandamano ya kupinga vita yaanza.
24 Septemba 2005Maelfu kadha ya waandamanaji wameanza kuandamana kupitia eneo la kati la mji wa London leo Jumamosi wakitaka kumalizwa kwa vita vinavyoongozwa na Marekani dhidi ya Iraq na kurejeshwa kwa wanajeshi wa Uingereza walioko katika nchi hiyo.
Maandamano hayo yakupiga vita pia yamepangwa kufanyika katika miji wa Roma, Italia, Paris Ufaransa, Madrid nchini Hispania na Copenhagen Denmark , pamoja na Oslo Norway na Helsinki Sweden.
Muungano wa kusitisha mapigano , ambao ndio uliotayarisha maandamano hayo ya mjini London kwa kushirikiana na kundi linalofanya kampeni ya kuondoa silaha za kinuklia pamoja na Jumuiya ya Kiislamu nchini Uingereza, wamesema kuwa wanatarajia kiasi cha watu wapatao 100,000 watashiriki maandamano hayo.
Waandamanaji walijikusanya nje ya jengo la bunge kabla ya kuanza maandamano yao na kwenda katika eneo la Hyde Park.
Baadhi ya waandamanaji wamebeba mabango yanayomshutumu waziri mkuu Tony Blair kwa udanganyifu na kumtaka ajiuzulu.
Wakati huo huo kiongozi wa chama kikuu cha kisiasa cha Washia nchini Iraq ametoa wito nae pamoja na miito ya viongozi wa kidini wanaotaka kura ya ndio kwa ajili ya muswada wa katiba mpya ya nchi hiyo, wakati waandamanaji nchini Marekani na Ulaya wakiandamana dhidi ya vita nchini Iraq.
Na katika mji wa kusini mwa Iraq wa Basra, jaji ametoa hati ya kukamatwa wanajeshi wawili wa Uingereza ambao waliokolewa na wanajeshi wenzao katika operesheni ya kutatanisha mapema wiki hii, kwa madai ya kumuua polisi mmoja wa Iraq.