LONDON. Kituo Al jazeera chamuonyesha mtuhumiwa wa shambulio la bomu la julai nchini Uingereza
2 Septemba 2005Matangazo
Mtuhumiwa mmoja kati ya watuhumiwa wanne wa mashambulio ya bomu ya julai katika mji wa London nchini Uingereza, ameonyeshwa katika televisheni ya kiarabu ya Al Jaazera akizungumzia juu ya shambulio hilo na kusema, kwamba kushiriki kwa Uingereza katika vita ya Irak ndio sababu hasa iliyo pelekea shambulio hilo kufanyika.
Mohammad Sidique Khan pia alionya mashambulio zaidi katika bara la Ulaya.
Mara baada ya kituo cha Al Jazeera kuonyesha ukanda wa video juu ya mtuhumiwa huyo kilimuonyesha pia naibu wa Osama bin Laden, Ayman al Zawahri ambae alisema wazi wazi kuwa kundi la al Qaeda ndio lililo husika na mashambulio ya mjini London ya mwezi julai, watu 52 waliuwawa.