LONDON: Hakuna maafikiano kuhusu miradi ya kinuklia ya Iran
30 Aprili 2005
Iran imetishia kuanzisha upya mradi wa kuimarisha madini ya uranium,baada ya kukwama kwa majadiliano yake pamoja na wapatanishi wa Umoja wa Ulaya mjini London.Pande hizo mbili zinatazamiwa kukutana tena wiki ijayo.Ujerumani,Ufaransa na Uingereza zinajaribu kuishawishi Iran iachilie mbali kabisa miradi yake ya kinyuklia na badala yake Iran itapewa vichocheo vya kiuchumi na kisiasa.Serikali ya Tehran imesitisha kwa muda mradi wake wa kurutubisha madini ya uranium,kuonyesha kuwa ipo tayari kutafuta suluhisho.Lakini serikali hiyo inataka kupewa uhakika kuwa chini ya uangalizi,itaruhusiwa kuendelea na mradi wake wa kuimarisha madini ya uranium kwa kiwango fulani.Iran daina imekanusha madai ya Marekani kuwa kwa siri inatenegeneza silaha za kinuklia.