LONDON. Askari wa Uingereza wazidi kuuawa Irak.
2 Mei 2005Wizara ya ulinzi ya Uingereza imethibitisha kwamba askari wake mmoja ameuawa leo nchini Irak na hivyo kufanya idadi ya askari wa Uingereza waliouawa katika vita ya Irak kufikia 87.
Uingereza ina askri alfu nane na mia saba nchini Irak.
Wakati huo huo suala la Irak linatarajiwa kutamalaki katika agenda ya uchaguzi mkuu nchini Uingereza ambapo waziri mkuu bwana Tony Blair anatarajiwa kupita kwa mara ya tatu.
Na wizara ya ndani ya Irak imefahamisha kwamba kamanda wa polisi jenerali Rashid Flaih leo ameponea chupu chupu kuuawa baada ya bomu lililotegwa ndani ya gari kuripuka karibu na msafara wake wa magari kaskazini mwa mjini Baghdad.
Hatahivyo baadhi ya wapambe wake walijeruhiwa katika shambulio hilo.
Habari zaidi zinasema kwamba raia wanne pia walijeruhiwa miongoni mwao akiwamo mtoto mmoja.