LOME :Machafuko ya Togo yameuwa watu 400 hadi 500
27 Septemba 2005Matangazo
Vikosi vya usalama nchini Togo kwa kiasi kikubwa vinapaswa kulaumiwa kwa ghasia kuhusiana na uchaguzi wa mwezi wa April ambapo kwayo watu 400 hadi 500 wameuwawa.
Kamishna wa Umoja wa Mataifa wa Haki za Binaadamu Louise Abhor amesema ujumbe maalum kwa taifa hilo la Afrika Magharibi umegunduwa ushahidi wa kuwepo kwa mauaji holela, utesaji na vitendo vyengine kinyume na ubinaadamu wakati na baada ya uchaguzi wa Rais nchini humo.
Kwa mujibu wa repoti ya Umoja wa Mataifa baadhi ya wahanga waliuliwa hapo kwa papo wakati wengine walikatwa na mapanga au kupata mkon’goto wa marungu,kuchomwa misumari kwenye makucha na wanawake kadhaa kubakwa.