LOJA JIRGA lafikia muwafaka wa katiba Afghanistan
4 Januari 2004Matangazo
KABUL: Nchini Afghanistan, Baraza Kuu la Bunge limefikia muwafaka wa katiba baada ya mashauriano yaliyodumu majuma matatu, aliarifu Rais wa Baraza, LOYA JIRGA Sebghatullah Mujaddidi. Mwanachama wa Baraza hilo Safia Sidiki alisema umeweza kuwekwa kando ule mvutano kuhusu lugha rasmi ya kiserikali. Kwa sababu hiyo huenda kikamalizika leo leo kikao cha Baraza hilo. Mpaka dakika ya mwisho wajumbe hawakuweza kuwafikiana juu ya swali iwapo Kiuzbeki kinachosemwa Afghanistan ya Kaskazini kiwe lugha ya tatu rasmi pamoja na Kipashtu na Kidari.