Wakoloni wa Kijerumani walipoingia Afrika Mashariki, walikutana na nguvu ambayo hakuna aliyekuwa ameitarajia ya Li'ti Kidanka. Li’ti Kidanka alikuwa kiongozi wa kiroho kutoka jamii ya kabila la WaNyaturu mkoani Singida, kanda ya Kaskazini-Kati mwa Tanzania.